Script 1
[Rekodi hii itatumiwa kwenye IVR. Tungependa iwe yenye kushirikisha]
Jambo! Asante kwa kupigia kampuni yetu! Njia bora ya kupata sauti mwafaka kwa ajili ya mradi wako katika kila lugha!
Ili kujua mengi zaidi kuhusu kampuni yetu, bonyeza moja.
Ikiwa ungependa kuwasilisha mradi au kuzungumza na timu yetu ya mauzo, bonyeza mbili.
Unahitaji usaidizi kutoka kwa timu yetu inayosimamia uzalishaji?
Hakuna shida! Tafadhali bonyeza tatu.
Kwa maswali yanayohusu ubora, bonyeza nne.
Una mawazo yoyote? Mapendekezo? Tungependa kuyasikiliza! Bonyeza tano.
[Tafadhali soma hii kana kwamba unanong’oneza] Psst! Wataka kuwa sehemu ya timu yetu?
[Rudi kwenye sauti ya kawaida] Tunaajiri!
Tafadhali tembelea tovuti yetu ili ujifunze mengi kuhusu nafasi za ajira zilizoko kwa sasa!
Script 2
[Rekodi hii itatumiwa katika video yetu ya kampeni ya uhamasishaji. Tunataka isisimue, ifurahishe na istaajabishe kidogo.]
Katika ulimwengu ambao sauti ambatanishi ilikuwa vigumu kupata, katika ulimwengu ambao jitihada na gharama nyingi zilihitajika ili kufuatilia kazi maisha ya kaimu sauti; tuliamua kuanzisha mapinduzi!
Safari hiyo haijawa rahisi, lakini tumeimarika kuliko wakati mwingine wowote.
Hatua kwa hatua, tumeunda huduma ya kidijitali ili kukuletea kiwanda cha sauti ambatanishi kwako nyumbani. Tumekuhusisha katika misheni hii na twatarajia utashiriki katika ndoto hii.
Hakuna kutazama nyuma.
Tulikuja, Tulibadili ulimwengu, na tuko hapa [Tua kidogo hapa] kudumu.
Tunaleta kiwanda cha sauti ambatanishi mikononi mwako.
Script 3
[Rekodi hii itatumiwa kwenye video yetu ya bidhaa. Tunataka iwe thabiti, yenye kusisimua na fasaha]
Kwa nini sisi ndio chaguo bora ya kujipatia sauti ambatanishi za wataalamu?
Kwanza tunawasilisha tu sauti ambatanishi ambazo zimechunguzwa kwa kina na timu yetu ya kudhibiti ubora. Isitoshe, kundi letu la wasanii wa sauti ambatanishi wana maelfu ya chaguo kwa ajili yako katika lugha nyingi, mitindo na bei linganifu! Zaidi ya yote hayo, Miradi yetu imeimarishwa na uhakikisho wetu wa uradhi, ikiwa hautapendezwa na matokeo, timu yetu inayosimamia uzalishaji itaingilia kati na kukurudishia pesa zako. [Tua kidogo baada ya kila neno] Hakuna maswali.
Sisi ni washupavu inapohusu kuwasaidia wateja; timu yetu inafurahia kusaidia. Tunahakikisha kwamba uhusiano baina yetu ni endelevu, wa kitaalamu, [Tua kidogo hapa] na unaofurahisha!